SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA (TBS) KWA UFUPI
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ni Shirika la Umma chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, lililoundwa chini ya Sheria ya Bunge Nambari 3 ya mwaka 1975 na kurekebishwa chini ya Sheria Namba 1 ya mwaka 1977.

MAJUKUMU YA TBS
TBS ina majukumu makuu manne:

  • Kuweka na kusimamia viwango vyote vya kitaifa.

  • Kutoa ushauri viwandani juu ya uzalishaji wa bidhaa bora.

  • Kupima na kuhakikisha vipimo vinavyotumika viwandani.

  • Kuelimisha umma juu ya masuala yote yanayohusu uwekaji na usimamiaji wa viwango pamoja na udhibiti wa ubora wa bidhaa viwandani.

VIWANGO VYA TANZANIA
Viwango vya Tanzania ni viwango vya kitaifa vilivyokwishawekwa au vitakavyowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na. 3 ya mwaka 1975 vikielezea kanuni za uzalishaji, uhifadhi na ufungashaji wa bidhaa bora.

Mpaka sasa TBS imeishaandika viwango zaidi ya 1000 katika nyanja za Kilimo na Chakula, Ngozi, Kondom, Madawa, Nguo, Uhandisi mitambo, Uhandisi ujenzi na Uhandisi umeme.

UTEKELEZAJI WA VIWANGO

Viwanda kadhaa hapa nchini, vya serikali pamoja na vya watu binafsi, hufuata na kutumia viwango vya kitaifa katika uzalishaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali nchi za nje.

Ili wananchi waweze kufaidika na viwango, TBS inaendesha mpango wa uthibiti wa ubora wa bidhaa, ambao unaliwezesha Shirika kutoa leseni kwa wazalishaji bidhaa wanaothibitishwa kuwa wanazalisha kulingana na kiwango cha kitaifa cha bidhaa husika ambayo huwaruhusu kutumia alama ya ‘’tbs’’ ya ubora wa bidhaa.

FAIDA ZA VIWANGO

  • Huweka usawa katika uwanja wa biashara

  • Huondoa mkanganyiko kuhusiana na bidhaa

  • Husaidia kufungua masoko zaidi

  • Hurahisisha biashara baina ya nchi na nchi

  • Hutoa uhakikisho wa ubora, usalama, kuaminika na ufanisi

  • Huipa serikali urahisi wa kuunda sheria zinazohusiana na masuala ya afya, usalama na uhifadhi wa mazingira

  • Hulinda afya na usalama wa walaji/watumiaji wa bidhaa mbalimbali.

FAIDA ZA ALAMA YA UBORA YA 'tbs'

Kwa mteja/mlaji

  • Humthibitishia kuwa bidhaa husika inafaa kwa matumizi husika

  • Huwezesha kupungua kwa bei ya bidhaa kutokana na ushindani

  • Humhakikishia usalama wake kiafya na katika matumizi

  • Huongeza ubora wa maisha

  • Hulinda mazingira yake.

Kwa mzalishaji

  • Humpa uwezo mkubwa zaidi wa kushindana sokoni

  • Humpatia wateja zaidi

  • Humwondolea usumbufu wa kupima bidhaa kwa kuzingatia matakwa ya mnunuzi

  • Humkinga dhidi ya ushindani na bidhaa duni zisizo na viwango.

MAABARA
TBS ina maabara saba zenye vifaa vya kisasa na wataalamu wa kutosha katika nyanja za madawa, kilimo na chakula, nguo/kondom/ngozi, uhandisi mitambo, uhandisi ujenzi, na uhandisi umeme pamoja na maabara ya ugezi.

Kwa maelezo zaidi tuandikie kwa kutumia anwani hii:

Shirika la Viwango Tanzania
S L P 9524 Dar es Salaam
Tanzania


Simu: +255 22 2450206 / +255 22 2450949   Faksi:+255 22 2450959

Barua pepe:info@tbstz.org   Tovuti: www.tbstz.org

Au tuone katika eneo la UBUNGO, Dar es Salaam kwenye kona ya Barabara za Morogoro na Sam Nujoma.
                                                                                                                                                   (
Read more about TBS Services)
[
Top]


 
 

Home  |  About TBS   |   TBS kwa Ufupi   |   TBS Administration  |  TBS Services  |  TBS Publications  |  News and Events  |  Links   |  Vision  |  Contact us

© Copyright 2008  All Rights Reserved www.tbstz.org